Walinzi wa Lamu

Uchunguzi wa Kampeni dhidi ya Mradi wa Makaa ya Mawe wa Lamu

Desemba 2024

Mnamo mwaka 2013, serikali ya Kenya ilitangaza mipango ya kujenga kituo kikubwa cha kuzalisha meme wa makaa ya mawe cha megawati 1050 katika kaunti ya Lamu, eneo la Kwasasi, kama sehemu ya mkakati wa Viwanda wa Vision 2030. Mradi huo wa Dola za Marekani bilioni 2, uliopangwa kutekelezwa na kampuni ya Amu Power, ulitishia Mji wa Kale wa Lamu, linalotambuliwa na UNESCO kwa uhifadhi wa tamaduni za tangu jadi, turathi pamoja na bioanuwai yake ya kipekee, ikiwemo misitu ya mikoko na miamba ya matumbawe.

Zaidi ya wamiliki wa ardhi 600 walitarajiwa kupoteza makazi na maisha yao kutokana na ununuzi wa hekari 387 za ardhi kwa ajili ya mradi huo. Ingawa kampuni ya Amu Power katika mikutano zake, iliahidi ajira na ukuaji wa uchumi kwa jamii ya Lamu, mradi huo ulikosa uwazi na ushirikishwaji wa kina, ulipaji wa fidia wa kutosha, au mipango ya kuhama. Hatari za uchafuzi wa hewa, ardhi, na maji zilikuwa ni wasiwasi mkubwa kwa jamii. Hata hivyo, michango ya jamii ilipuuzwa; serikali na kampuni ya Amu Power walikosa kuchunguza suluhisho mbadala za nishati a tishio linalokaribia kwenye mfumo wa mazingira. Hi iliongeza hasira za wenyeji a kuwaunganisha kupinga mradi huu.

Uchunguzi huu unaelezea jinsi watu wa Lamu walivyoanzisha harakati za kijamii zilizowafanya wafadhili wakuu kujiondoa, na hatimaye kufuta leseni ya mazingira ya mradi huo. Soma zaidi kujifunza jinsi mafanikio haya yalivyopatikana, na vidokezo kwa wanaharakati wengine wanaopinga miradi yenye madhara inayofadhiliwa kimataifa.

Kutoka Uvumi hadi Ukweli:

Ugunduzi wa Jamii ya Lamu Kuhusu Mradi wa Makaa ya Mawe

Wakati wawakilishi wa Amu Power walipowasiliana na jamii ya Lamu kwa mara ya kwanza, waliwahakikishia ajira, ufadhili wa shule kwa watoto wao, na fidia kwa ardhi yao. Hata hivyo, hawakutafuta ridhaa wala maoni ya jamii, hali iliyoacha wakazi gizani kuhusu maelezo ya mradi huo. Wakulima wengi, ambao ardhi yao ilikuwa tayari imechukuliwa, hawakuelewa madhara au athari za mradi huo. Wanajamii waliokusanyika kama Save Lamu-ambayo baadaye ikawa muungano wa zaidi ya mashirika 40 ya jamii-walikusanya jamii ya Lam kuhakikisha wasiwasi wao unasikilizwa na Amu Power na watunga maamuzi wengine.

“Habari kuhusu mikutano ya ushirikishwaji wa umma haikuwasilishwa vizuri, na maeneo ya mikutano yalibadilishwa dakika za mwisho. Tulikusudia kuhudhuria mikutano na kuishinikiza Amu Power kutoa maelezo kamili kuhusu mradi huo.”

~Khadija Shekuwe

Mratibu wa Save Lamu

Guardians of Lamu A Case Study on the Campaign against the Lamu Coal Project December 2024

Tafuta taarifa kuhusu maelezo ya mradi haraka iwezekanavyo.

Jenga muungano wa mashirika ili kupunguza hatari kwa watu binafsi na mashirika.

Tembea na jamii katika kila hatua ya utetezi.

- Mikakati Kazini

Nguvu ya Jamii:

Hatua za Lamu za Kutetea Ardhi Yao na Mazingira

Baada ya kukosa majibu ya mana kutoka kwa mamlaka na Amu Power, Save Lamu walitambua haja ya kupanua juhudi zao za utetezi. Kwa kushirikiana na mashirika ya ndani na kimataifa, walitumia mbinu mbalimbali kupinga mradi wa makaa ya mawe. Mbinu hizi zilijumuisha kukusanya ukweli kuhusu mradi huo, kushirikisha jamii, kuongeza uelewa kupitia kampeni za vyombo vya habari, kuandaa maandamano ya amani, na kutafuta suluhisho kupitia mahakama na hatua zisizo za kisheria. Kwa kutumia mbinu hizi, jamii ilipinga mradi huo na kutetea ardhi yao, mazingira, na maisha yao.

a. Kujifunza na Kushirikisha: Masomo ya Kimataifa Yaliyoimarisha Uelewa wa Kijamii

Save Lamu walitambua haja ya kupinga taarifa potofu zilizokuwa zinasambazwa na Amu Power, ambao walidai kwamba mradi wa makaa ya mawe ungenufaisha jamii. Ili kufanya hivyo kwa ufanisi, walihitaji kukusanya ukweli kuhusu athari halisi za miradi ya makaa ya mawe. Mnamo mwaka 2019, Save Lamu waliandaa ziara za kubadilishana maarifa Afrika Kusini na India, ambapo wawakilishi wa jamii ya Lamu walipata fursa ya kuna kwa macho yao athari mbaya za uzalishaji wa makaa ya mawe. Ziara hizi zilijumuisha mikutano na waendeshaji wa mitambo ya makaa ya mawe, mazungumzo na jamii zilizoathiriwa, na kurekodi uharibifu wa mazingira uliosababishwa na miradi hiyo.

“Haikuwa mpaka nilipofika India ndipo nilipogundua ukubwa wa tatizo tulilokuwa tukikabiliana nalo. Athari za makaa ya mawe kwenye afya ya binadamu, viumbe vya baharini, mikoko, na ardhi zilikuwa za kutisha na zisizoweza kurekebishwa. Nilihisi hitaji la haraka kurudi Kenya na kusimamisha mradi huu.”

~Ustadh Mahmoud Abdulkadir

Mwanazuoni wa Kiislamu na Mjumbe wa Bodi ya Save Lamu.

“Tulichoona Afrika Kusini kilikuwa tofauti kabisa na yale ambayo Amu Power waliwaambia watu wetu. Kulikuwa na uchafuzi mkubwa wa taka, maji yaliyochafuliwa, na jamii zenye magonjwa. Tulitumia picha na video tulizokusanya kutengeneza nyaraka na kushirikisha jamii yetu kupitia mikutano ya hadhara.”

~Raya Famau

Mjumbe wa Bodi ya Save Lamu na Mwenyekiti wa Lamu Women Alliance.

Matokeo ya ziara hizi yalifichua jinsi miradi ya makaa ya mawe ilivyokuwa na madhara kwa afya ya binadamu, maisha ya baharini, na uchumi wa ndani. Kwa maarifa haya, Save Lamu waliimarisha juhudi zao za utetezi wa kijamii kwa kushirikisha taarifa kupitia mikutano ya hadhara, vipindi vya redio, mitandao ya kijamii, na uonyeshaji wa filamu hadharani. Walihakikisha kuwa ujumbe wao ulikuwa wazi, wa kweli, na ulitokana na uzoefu wa moja kwa moja wa jamii zilizoathiriwa na makaa ya mawe katika nchi nyingine.

“Nilitembea Afrika Kusini na India, na hali ilikuwa sawa katika maeneo yote mawili-umasikini, huzuni, na hakuna maendeleo ya kiuchumi halisi kutokana na uzalishaji wa makaa ya mawe. Tulizungumza na watu wa maeneo hayo, tukachukua video, na kukusanya nyenzo za kushiriki na jamii yetu”

~ Abubakar Mohammed

Mfanyabiashara wa Samaki na Mwenyekiti wa Pate BMU.

“Tulihakikisha ujumbe wetu ulikuwa wa ukweli na uliendana na matokeo ya utafiti wetu kuhusu makaa ya mawe. Picha na video za uzoefu wetu Afrika Kusini na India zilikuwa na athari kubwa sana. Zilichochea sana hadhira dhidi ya mradi wa makaa ya mawe, na ushuhuda wa wanajamii walioenda kwenye ziara pia uliwasisimua sana watu.”

~Hindu Salim

Mwanajamii Maendeleo ya Wanawake, Wadi ya Mkomani.

Save Lamu pia ilishirikiana na mashirika ya kimataifa kupinga mantiki ya kiuchumi ya mradi huo: utafiti ulionyesha kwamba kituo cha umeme wa makaa ya mawe kingekuwa kosa la gharama kubwa kwa Kenya, na kuwalemea watumiaji kwa gharama kubwa ya umeme kwa miaka mingi ijayo.

  • ⁍ Shirikiana na jamii zilizoathiriwa na miradi inayofanana na ungana na mitandao ya kikanda na kimataifa ili kupata maarifa na kujenga mshikamano. Ungana na vikundi vya mshikamano vya kikanda na kimataifa (kama vile African Coalition for Corporate Accountability na Coalition for Human Rights in Development) na waombe msaada kufanya utambulisho.
  • ⁍Tumia picha, video, na data kuimarisha ushahidi wako na shiriki matokeo na jamii yako ili kukuza uelewa na hatua.

  • ⁍Eneza maarifa kupitia mikutano, mitandao ya kijamii, na vyombo vya habari vya ndani ili kuwawezesha wanajamii kwa ufanisi.

b. Kutumia Mitandao ya Kijamii na Vyombo vya Habari kwa Mabadiliko

Mbali na kushiriki taarifa kuhusu mradi wa makaa ya mawe kwenye tovuti yao, Save Lamu ilikuwa hai sana kwenye majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, X (zamani Twitter), na YouTube. Matumizi ya mitandao ya kijamii yalisaidia sana katika kuhamasisha msaada wa ndani na kitaifa, kurekebisha simulizi la Amu Power kuhusu mradi huo, na kushirikisha jamii ya kimataifa.

Pia, walitumia mitandao hiyo kuwafikia watoa fedha wa mradi kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii. Kampeni hizi zilipata pia nafasi kwenye magazeti ya kitaifa na vipindi vya redio ambapo wanachama wa Save Lamu walibadilishana zamu kutoa wasiwasi wao kuhusu mradi.

Les gardiens de Lamu Une étude de cas sur la campagne contrele Projet de centrale à charbon de Lamu December 2024

“Kupitia mitandao ya kijamii, tuliweza kutoa taarifa za kila siku na kuwashirikisha hadhira pana zaidi katika mijadala kuhusu mradi wa makaa ya mawe. Baada ya kubaini wafadhili wa mradi, tuliwatambulisha kwenye machapisho yetu ili kuhakikisha wanajua wasiwasi wetu.”

~Mohammed Okeil

Msaidizi wa Mawasiliano wa Save Lamu.

Tumia mitandao ya kijamii kuwapa hadhira yako taarifa za mara kwa mara na
kuwashirikisha.

Tag wanahisa muhimu ili kuwalenga kwa ajili ya utetezi na kuimarisha ujumbe wako.

Tumia video na picha ili kuimarisha ujumbe wako.

c. Wito wa Lamu kwa Barua na Maombi ya Kupinga

Save Lamu ilituma barua kwa Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mazingira (NEMA), Idara ya Uvuvi, na Serikali ya Kaunti ya Lamu, ikieleza wasiwasi kuhusu mradi wa makaa ya mawe na ushiriki duni wa umma. Maombi pia yaliwasilishwa kwa Gavana wa Lamu, Issa Timamy, na Bunge la Kaunti, yakitaka mradi huo ukataliwe na kuzingatia mbadala wa nishati safi. Ingawa barua nyingi hazikujibiwa, maombi hayo yalisaidia kuweka kumbukumbu ya juhudi za jamii kuhusiana na mamlaka husika.

“Tuliandika barua na maombi kadhaa wakati wa kipindi cha utetezi. Kupitia hayo, tuliweza kujieleza bila hofu ya kupotoshwa au kutoeleweka. Pia tulitaka kuweka rekodi ya juhudi zetu na kujenga ushahidi wa kusaidia mikakati mingine kama maandamano na kesi za kisheria.”

~Adan Lali Kombo

Katibu wa Save Lamu

Guardians of Lamu A Case Study on the Campaign against the Lamu Coal Project December 2024

Kampeni hi ya barua ilipanuka zaidi ya mipaka ya kitaifa. Save Lamu pia iliwasilisha wasiwasi wao kwa vyombo vya Umoja wa Mataifa, kama vile Shirika la Umoja Mataifa (a Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), ambalo lilitambua Lamu Old Town kama makazi ya kale zaidi na yaliyo hifadhiwa vyema ya Waswahili Afrika Mashariki.
UNESCO hatimaye ilitoa wito wa kukomeshwa kwa mradi huo kutokana na athari hasi kwenye eneo la Urithi wa Dunia.

Boresha ujumbe wako ili kufanya madai maalum kwa ofisi sahihi.

Zingatia masala muhimu yanayohitaji kushughulikiwa.

Toa malengo yako kwa uwazi katika mawasiliano yote.

d. Maandamano ya Kulinda Mazingira

Save Lamu, kwa kushirikiana na mashirika ya kiraia na viongozi wa mitaa, waliandaa maandamano ya amani katika mji wa Lamu na Nairobi ili kupinga mradi wa makaa ya mawe. Maandamano hayo yaliunganisha makundi mbalimbali na kuimarisha harakati hizo, na hatimaye kusababisha kuundwa kwa vuguvugu la DeColonize ambalo lilileta umakini wa kikanda na kimataifa kwenye sababu yao. Licha ya vitisho na kukamatwa na serikali, ari ya jamii ilizidi kuimarisha juhudi zao za utetezi.

“‘Maandamano yalitupa nguvu. Kadri walivyotutesa, ndivyo tulivyotambua nguvu zetu za pamoja. Tulifanya kazi pamoja kama timu moja iliyo na lengo moja, bila kuruhusu maslahi binafsi kuzuia njia, haijalishi ni kwa muda gani mapambano yangechukua.”

~Walid Ahmed

Mwanamazingira na Mjumbe wa Bodi, Lamu Youth Alliance.

Maandamano ya amani ni njia nzuri ya kuvutia umakini wa watu na kueneza ujumbe wako.

Tarajia upinzani na vitisho lakini usikate tamaa. Pangilia mipango ya usalama na dharura ili kuwa tayari.

Shirikiana na makundi mbalimbali ya jamii ili kupata uungwaji mkono mpana.

e. Kupeleka Mapambano Mahakamani

Kwa niaba ya Save Lamu na wanajamii binafsi, mawakili wa Katiba Institute waliwasilisha ombi mahakamani kupinga hatua ya NEMA ya kutoa leseni ya mazingira kwa Amu Power. Timu ya mawakili, kwa msaada wa Natural Justice na Environmental Law Alliance Worldwide (ELAW), ilipinga ukamilifu wa ripoti, michakato, na maamuzi yaliyosababisha kutolewa kwa leseni hiyo.

Somo Mohamed Somo, Mohamed Mbwana, Adam Lali Kombo na Swaleh Elbusaidy kutoka Save Lamu walijiunga na DeCOALonize na mashirika mengine katika Bustani ya Central, Nairobi mwaka 2019 kupinga mradi wa makaa ya mawe.

Wanaharakati wa Lamu, Walid Ahmed na Ishaq Abubakar, wakiongoza maandamano katika ufuo wa bahari wa Lamu.

Guardians of Lamu A Case Study on the Campaign against the Lamu Coal Project December 2024

“Ripoti za NEMA zilikuwa ndefu na zilitumia lugha ya kitaalamu, jambo lililowafanya wanajamii kushindwa kuelewa kabisa athari za mazingira na kibailojia za mradi huu.

Pia tuliona kuwa ushiriki wa umma ulikuwa mdogo na taarifamuhimu ziliwekwa siri kwa walioathirika.”

~Lempaa Suyianka

Katiba Institute

“Tuligundua kuwa mashtaka ya kisheria ni zana yenye nguvu tunapokabiliana na miradi tata kama huu wa makaa ya mawe. Ikawa mbinu muhimu kuhakikisha mamlaka za umma zinawajibika kwa maamuzi yao.”

~Khadija Juma

Mkuu wa Mawasiliano, Save Lamu

Guardians of Lamu A Case Study on the Campaign against the Lamu Coal Project December 2024

Uamuzi wa kihistoria wa mahakama mnamo Juni 2019 ulithibitisha kuwa NEMA ilishindwa kuhakikisha ushiriki wa umma na kutathmini kwa usahihi hatari za mazingira, na hivyo kusababisha kufutwa kwa leseni ya mazingira ya mradi huo.
Ushindi huu wa kisheria ulisitisha ujenzi wa mradi na kuvutia umakini wa kimataifa.

Tumia hatua za kisheria kuimarisha utetezi wa jamii, inapofaa. Hatua za kisheria zinaweza kuwa chaguo lenye nguvu kuchelewesha au kusimamisha mradi huku utetezi mwingine ukiendelea.

Tafuta msaada wa wataalam kutafsiri ripoti za kiufundi na kubaini ukiukwaji.
Mashirika kama Environmental Law Alliance Worldwide (ELAW) yanaweza kukupa msaada wa kisheria na kisayansi.

Tangaza kila hatua ya juhudi zako za kisheria na utetezi kupitia vyombo vya habari.

f. Kufuata Wafadhili

Kuelewa kuhusu wafadhili wa mradi kulisaidia Save Lamu kuwasiliana waziwazi kupinga kwao mradi huo na kudai wafadhili waache kuunga mkono kifedha mradi huo.

i. Kuelewa Ufadhili wa Mradi

Uelewa wa jinsi mradi unavyofadhiliwa ni muhimu katika kusaidia jamii kuelewa chanzo cha pesa na jinsi ya kupinga mradi usiofaa. Save Lamu, kwa msaada wa washirika wake, iliweza kufuatilia na kubaini wafadhili wa mradi wa makaa ya mawe.
Wafadhili waliobainika ni pamoja na Centum Investment Group, Benki ya Kibiashara ya Viwanda ya China (ICBC), Standard Bank, FirstRand Bank ya Afrika Kusini, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC).

Guardians of Lamu A Case Study on the Campaign against the Lamu Coal Project December 2024

“Amu Power haikutoa taarifa kuhusu wafadhili wa mradihadharani. Ilibidi tufanye utafiti mwingi na Kupata msaada kutoka kwa mashirika washirika ili Save Lamu iweze kubaini ni nani waliokuwa wakiunga mkono kifedha mradi huu.”

~Khadija Juma

Communications Officer, Save Lamu

“Tulitambua baadaye kwamba juhudi zetu za utetezi zingekuwa na ufanisi zaidi kama tungewatambua wachezaii wakuu kutoka mwanzo.”

~Adam Lali Kombo

Board Member, Save Lamu

Guardians of Lamu A Case Study on the Campaign against the Lamu Coal Project December 2024

Fanya utafiti na tambua wafadhili wa mradi mapema ili kuelekeza mkakati wako wa utetezi.

Usisite kutafuta msaada.Follow The Money ya Inclusive Development International na The Counter ya SOMO vinaweza kusaidia na utafiti wa kampuni na uelewa wa uwekezaji.

Dai uwazi kutoka kwa waendeshaji wa mradi kuhusu ufadhili wao.

ii. Kuishawishi Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)

Save Lamu walijifunza kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ilikuwa inafikiria kutoa dhamana ya hatari ya dola milioni 100 kwa mradi wa makaa ya mawe wa Lamu. Ili kushughulikia hili, Save Lamu waliwasiliana kwanza na benki kupitia barua, wakielezea wasiwasi wao kuhusu athari za mazingira na kijamii za mradi huo. Mnamo Mei 2018, kwa msaada wa washirika, Save Lamu ilifanikisha ushiriki wa wanachama wake wawili katika Jukwaa la Kiraia la AfDB lililofanyika Abidjan. Hapo, walijadiliana na wajumbe wa bodi ya benki hiyo kuhusu masala yanayoendelea, hususan ukosefu wa tathmini sahihi za athari za mazingira na kijamii za mradi wa makaa ya mawe.

“Katika Jukwaa la Kiraia la AfDB huko Abidjan, mwanzoni hatukuwa na uhakika wa jinsi maafisa wangechukua wasiwasi wetu. Hata hivyo, tulishangazwa vyema na jinsi walivyotushirikisha. Walisikiliza kwa makini, na majibu yao yalituhakikishia kuwa juhudi zetu zinaendelea na kwamba
hatupigani bure”

~Raya Famau

Mjumbe wa Bodi ya Save Lamu na Mwenyekiti wa Lamu Women Alliance.

Walinzi wa Lamu Uchunguzi wa Kampeni dhidi ya Mradi wa Makaa ya Mawe wa Lamu

Hatimaye, AfDB ilisitisha uamuzi wake wa awali wa kutoa dhamana ya hatari kwa mradi huo. Kufikia Novemba 2019, benki hiyo ilitangaza rasmi kwamba haitafadhili mradi wa makaa ya mawe wa Lamu na kwamba haina mipango ya kufadhili miradi ya makaa ya mawe siku za usoni.

Shirikiana na taasisi za kifedha mapema ili kuzuia miradi hatari.

Tumia majukwaa ya kiraia kukutana na maamuzi ya moja kwa moja kutoka kwa
watoa maamuzi.

Sherehekea mafanikio madogo ili kudumisha kasi ya utetezi.

iii. Kuwajibisha Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC)

Mnamo mwaka wa 2019, kupitia ufuatiliaji wa mlolongo wa uwekezaji, Save Lamu waligundua kuwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) la Benki ya Dunia lilihusishwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja katika kufadhili mradi wa makaa ya mawe wa Lamu. Ushiriki huu ulitambuliwa kupitia mahusiano ya kifedha ya kati na Benki ya Kibiashara ya Kenya, Benki ya Ushirika ya Kenya, na Benki ya FirstRand ya Afrika Kusini, zote ambazo zilitoa ufadhili kwa Centum Group, kampuni mama ya Amu Power.

Kwa kutumia habari hii, Save Lamu na Kundi la Kujisaidia la Wakulima wa Kwasasi Mvunjeni waliwasilisha malalamiko kwa Compliance Advisor Ombudsman (CAO). Malalamiko hayo yalielezea wasiwasi kuhusu uvunjaji wa Mfumo wa Uendelevu wa IFC, hasa kwa kuonyesha ukosefu wa tathmini kamili ya Athari za Mazingira na Kijamii (ESIA). Malalamiko hayo yalionyesha kutokuwepo kwa mashauriano ya kutosha na jamii zilizoathirika, upungufu wa mipango ya uhamishaji, na hatari za mazingira kama uchafuzi wa hewa na maji, pamoja na vitisho kwa urithi wa kitamaduni wa Lamu, ikiwemo ukaribu wake na tovuti ya Urithi wa Dunia wa UNESCO. Jamii pia ilikosoa ukosefu wa uchunguzi wa vyanzo vingine vya nishati isiyo na madhara na kushindwa kufanya tathmini ya athari za pamoja za mradi wa LAPSSET unaohusishwa na mradi wa makaa ya mawe.

Accountability Counsel inasaidia jamii kuibua masuala ya kijamii na mazingira dhidi ya miradi hatari inayofadhiliwa na wawekezaji wa kimataifa, huku wakiwaongoza kupitia mifumo huru ya uwajibikaji ili kusimamisha ukiukaji wa haki na kupata fidia pale ambapo madhara yametokea.”

~Robi Chacha Mosenda

Afisa Mwandamizi wa Jami, Afrika, Accountability Counsel.

Licha ya wasiwasi uliotolewa, CAO ilikataa malalamiko hayo, ikieleza kuwa ushiriki wa IFC kupitia waingiliaji wa kifedha haukuwa na athari ya moja kwa moja kwenye mradi huo. Ingawa hi ilikuwa pigo kwa jamii, mchakato huo ulisaidia kuongeza ufahamu miongoni mwa wafadhili kuhusu wasiwasi wa jamii. Hii ilisababisha IFC kuchukua hatua za kupunguza au kumaliza uhusiano wake na benki zinazofadhili mradi huo makaa ya mawe. Kesi hii pia ilionyesha changamoto za kuwajibisha taasisi za kifedha za kimataifa wakati fedha zinatoka kupitia benki za ndani na kikanda, hali iliyochangia mabadiliko ya sera yanayohitaji uwazi zaidi wakati IFC inafadhili miradi yenye hatari kubwa kama ule wa makaa ya mawe wa Lamu.

Fikia wataalamu kama Accountability Counsel ili kusaidia katika kutumia mchakato wa Mfumo Huru wa Uwajibikaji (IAM)

Fikiria kutumia mifumo ya uwajibikaji pale ambapo mradi umefadhiliwa na wawekezaji wa kimataifa.

Kuweka kumbukumbu za wasiwasi wa Jami kunarahisisha kutoa taarifa zinazolingana na zenye mvuto wakati wa mchakato wa IAM.

iv. Kuwashawishi ICBC Waachane na Mradi wa Makaa

Baada ya kubaini kwamba Benki ya Viwanda na Biashara ya China (ICBC) ilikuwa mfadhili mkuu wa mradi wa makaa ya mawe, Save Lamu ilianza kufanya kazi na washirika kushirikiana na ICBC kupitia mkakati wa mawasiliano ya barua pepe. Ingawa hawakupokea majibu mwanzoni, Save Lamu ilivumilia.

Mnamo Juni 2019, Save Lamu, Vuguvugu la DeCoalonize, na wanamazingira wengine waliandaa maandamano katika Ubalozi wa China jijini Nairobi, wakilenga kuzishinikiza taasisi za kifedha za China, hususan ICBC, kuacha kufadhili mradi wa makaa ya mawe wa Lamu. Maandamano hayo yaliongoza kwenye mkutano na Ubalozi wa China na wadau wengine, lakini ICBC haikuhudhuria. Bila kukata tamaa, Save Lamu iliendelea na juhudi zake za kufikia ICBC, mfadhili mkuu wa kifedha wa mradi huo.

Baada ya miaka ya juhudi za utetezi, Save Lamu hatimaye iliweza kufikia CBC kupitia makati uliounganisha matumizi ya mitandao ya kijamii, mawasiliano ya barua pepe, nyaraka za kina za wasiwasi wa jamii, na mijadala ya hadhara ili kuwashinikiza benki kuwajibika kwa kufadhili mradi huo wa makaa ya mawe. Juhudi za uvumilivu za Save Lamu zilifanikiwa mnamo Novemba 2020, wakati ICBC ilipothibitisha kuwa imeacha mpango wake wa kufadhili mradi wa makaa ya mawe wa Lamu.

“Tulijaribu kuwasiliana na ICBC kupitia barua pepe na Balozi wa China bila mafanikio. Barua pepe zetu nyingi zilirudi bila kufikishwa, na ICBC hawakuwa na ofisi ya ndani hapa Kenya,
hali iliyozidisha ugumu. Hatimaye, tulipata anuani za mawasiliano ya wafanyakazi wakuu wa ICBC katika ofisi yao ya Ulaya. Tuliongeza kasi ya mawasiliano kupitia barua pepe hadi baada ya karibu miaka miwili, CBC ilituandikia kuthibitisha kujiondoa kwao katika mradi huo.”

~Mohammed Athman

Mjumbe wa Bodi ya Save Lamu

Kuwa na uvumilivu katika juhudi zako za mawasiliano. Kutokupata jibu haimaanishi kuwa mawasiliano yako hayafanyi kazi.

Tumia mahusiano na mitandao kupanua utetezi wako ili kufikia walengwa ambao huwezi kuwafikia moja kwa moja. Tafuta usaidizi kutoka kwa washirika wenye uzoefu wa kushirikiana na wahusika wa Kichina ili kupata mawasiliano sahihi na kujua jinsi ya kuwafikia..

Endelea kushinikiza wafadhili wakuu wa kifedha wa mradi. Pesa ni nguvu.

- Hitimisho

Mapambano Bado Yanaendelea:

Ushindi na Changamoto za Lamu

“Mapambano bado hayajaisha. Bado tunakabiliwa nachangamoto, hasa masala ambayo hayajatatuliwa kama vile kufurushwa kwa wakulima wa Kwasasi na ubadilishaji wa matumizi ya ardhi unaofanywa vibaya na Tume ya Kitaifa ya Ardhi na Serikali ya Kaunti. Ingawa mradi wa makaa ya mawe ni sehemu ya mpango wa Vision 2030 wa serikali, ni lazima tuendelee kupigania suluhisho la nishati endelevu ambalo litalinda mazingira ya Lamu na kuzingatia ustawi wa watu
wake.”

~Somo N. Somo

Mwenyekiti wa Save Lamu.

Les gardiens de Lamu Une étude de cas sur la campagne contrele Projet de centrale à charbon de Lamu December 2024

Uamuzi wa mahakama wa kufuta leseni ya mazingira ya mradi huo, ukosoaji wa UNESCO kuhusu mradi wa makaa ya mawe wa Lamu, na kujiondoa kwa wafadhili mbalimbali ulithibitisha juhudi za muda mrefu zilizofanywa na Kundi la Wakulima wa Kwasasi Mvunjeni, Save Lamu, DeCoalonize, na watu wa Lamu.

Mapambano haya dhidi ya mradi unaoungwa mkono na serikali yaliangazia nguvu ya kuandaa jamii, athari za utetezi unaotegemea ushahidi, na umuhimu wa ushirikiano wa wadau wengi katika kupinga miradi hatari inayoendeshwa na serikali na mashirika ya kimataifa.

Uvumulivu wa Save Lamu ni kumbusho muhimu kwamba, ingawa juhudi za uwajibikaji zinaweza kuchukua muda na kuwa ngumu, zinafaa kuendelezwa. Wanatumaini kwamba mafanikio yao yatatoa msukumo na nguvu kwa jamii kote ulimwenguni kulinda ardhi yao, haki zao, na mazingira yao.

Uchunguzi wa Kampeni dhidi ya Mradi wa Makaa ya Mawe wa Lamu